Dodoma, Machi 13, 2025 – Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa onyo kwa baadhi ya vijana wanaogushi cheti cha jeshi hilo kwa ajili ya kupata ajira kwenye taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 13, 2025, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Juma Mrai, amesema kuwa jeshi hilo limebaini uwepo wa vyeti feki ambavyo vimegushiwa na baadhi ya vijana ili wapate ajira katika taasisi za Serikali na binafsi.
Kanali Mrai amesema kuwa vijana hao wanagushi vyeti hivyo kutokana na baadhi ya taasisi na makampuni ya Serikali na binafsi kuweka utaratibu wa kutoa ajira kwa vijana kwa kuangalia kigezo cha sifa ya kupitia katika mafunzo ya JKT.
Aidha, Kanali Mrai amesema kuwa wale wote waliobainika na watakaobainika kugushi cheti cha jeshi hilo kwa matumizi yoyote yale, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Leave a Reply