Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo amewataka Vijana kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na Serikali ikiwemo mikopo ya Halmashauri ya 10%, huku akisema kuna fursa ambayo Vijana wengi hawaifahamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inampa fursa Kijana mwenye wazo na andiko zuri la biashara kupata hadi mkopo wa hadi Tsh. milioni 50.
Akiongea na Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Dar es salaam Tawi la UVCCM Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala, Jokate amesema “Niwasihi tuendelee kuomba mikopo kupitia kupitia mifuko inayowezesha Vijana kiuchumi ikiwemo mikopo ya Halmashauri 10%, lakini sijui kama mna taarifa kwamba Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi wanayo pia mifuko mbambali ya Vijana, siasa lazima iendane na uchumi”
“Tuna mifuko miwili ya Ofisi ya Waziri Mkuu inayowezesha kumkopesha Kijana mmoja mpaka Tsh. milioni 50, ukiwa umeandaa andiko lako wazo lako vizuri, hii ndio kazi ya Vijana kuambiana, lazima Vijana wajue kwamba kuna mifuko iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya kuwawezesha kujkwamua, kachukueni hizi fursa Vijana, msipozichukua nyie watachukua wengine, kama kuna Mtu yupo tayari tupo tayari kumsemea kumsaidia azipate”
“Tunatamani kuona Vijana wanaojitegemea kiuchumi ambao sio omba omba, ambao sio tegemezi, Rais Samia hataki kuona Vijana tegemezi ndio maana anatengeneza mfumo mzuri, Viongozi tuwaunganishe Vijana na hizo fursa, tunapeana michongo
Leave a Reply