Mwanafunzi ajirusha Ghorofani Zanzibar, Polisi waendelea na Uchunguzi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa huo ACP Abubakar Khamis limesema linaendelea kufatilia taarifa za Mwanafunzi wa Chuo cha IT MADRAS mwenye asili ya Kihindi aliyejirusha kutoka Ghorofani Zanzibar

Kamanda Abubakar ameeleza hayo wakati akijibu swali la mwaandishi wa habari aliyetaka kufahamu chanzo cha kijana huyo kujirusha

ACP Abubaka amesema tukio hilo ambalo limeripotiwa kutokea Jana April 16, 2025 linaendelea kuchunguzwa ili kubaini Mwananfunzi huyo alikua anasumbuliwa na nini hadi kufanya uamuzi huo