RC Chalamila aeleza sababu za Heche kukamatwa Kariakoo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefafanua sababu za kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, katika eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaam Aprili 22, 2025.

RC Chalamila, amesema Heche alikamatwa kwa kukiuka sheria kwa kuendesha mkutano wa hadhara katika eneo lisiloruhusiwa kisheria, Pia amesisitiza umuhimu wa wanasiasa kuheshimu taratibu za kufanya mikutano ya hadhara. Aliongeza kuwa serikali itachukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayekiuka sheria.

Kuhusu tetesi za maandamano yaliyopangwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu, Chalamila amesema vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kuhakikisha amani inadumishwa, huku akiwataka wananchi kufuata sheria na kuepuka kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali.