Jeneza la Papa Lafungwa Rasmi Katika Ibada ya Faragha Vatican

Jeneza lenye mwili wa marehemu Papa Francis limefungwa rasmi katika ibada ya faragha iliyohudhuriwa na viongozi wa Vatican na baadhi ya wanafamilia wa Papa.

Shughuli hiyo imefanyika baada ya waombolezaji zaidi ya 150, 000 kujitokeza kutoa heshima zao kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki katika Basilica la St. Peter.

Baada ya ibada hiyo ya kufunga jeneza kumalizika, Jumuiya ya St Peter itafanya ibada ya maombi mbele ya jeneza usiku kucha, hadi ibada ya mazishi itakapoanza kesho asubuhi.

Tukio hili linaashiria hatua nyingine muhimu katika maandalizi ya mazishi ya Papa Francis, huku Vatican ikiendelea kupokea wageni mbalimbali kutoka duniani kote watakaoshiriki katika ibada ya kesho.