Rais Samia apokea ujumbe wa Hayati Papa Francis

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa unyenyekevu ujumbe wa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Hayati Papa Francis, alioutuma kwake na kwa Watanzania wote kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano jana Aprili 26,2025.

Rais Samia amesema Papa aliandika Ujumbe huo siku chache kabla ya kufariki dunia na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino

“Kwa unyenyekevu na shukrani, nimepokea ujumbe wa Hayati Papa Francisko kwangu, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote aliouandika siku chache kabla Mwenyezi Mungu hajamwita kwake, na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino.”

“Tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu alale mahali pema” ✍️ – Rais @Samia_Suluhu_Hassan

Papa Francis alifariki dunia Aprili 21, 2025 akiwa na umri wa miaka 88, Mazishi yake yalifanyika jana Aprili 26, 2025 Roma, Italia.