Rais Mwinyi awaweka kikaangoni watakaoleta Urasimu kukwamisha biashara Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameahidi kwa Serikali kuviondoa Vikwazo vyote vinavyochangia Kukwamisha Uendeshaji wa Biashara hapa nchini.

Rais Dkt,Mwinyi ametoa Tamko Hilo alipoizindua Sera ya Biashara ya 2024 na Tathmini ya Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara (Zanzibar Blue Print) 2025 Hafla iliofanyika New Amani Hotel , Wilaya ya Mjini.

Dkt, Mwinyi amebainisha kuwa bado lipo Tatizo la kuwepo kwa Urasimu,Ucheleweshaji wa Watu kufanya Biashara zao na Utendaji usio na Ufanisi kwa baadhi ya Watendaji katika Sekta ya Biashara.

Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali haiwezi Kuendelea na Watendaji wanaosababisha kuwepo kwa Vikwazo katika Uendeshaji wa Biashara.

Amefahamisha kuwa mbali ya kuwepo kwa Vikwazo vya Kisheria ,Maingiliano ya Kisekta katika Utendaji pia lipo Tatizo la Utendaji unaokwamisha Biashara Jambo ambalo Serikali itahakikisha inawatambua. Watendaji hao na kuwaondoa.

Aidha amewatoa hofu Wadau na Taasisi zinazosimamia Sekta ya Biashara kuwa Serikali imedhamiria kuweka Mazingira mazuri ya Ufanyaji wa Biashara.

Rais Mwinyi ameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa Sera ya Biashara na Ripoti ya Tathmini lazima kuwepo na Msimamizi Mwenye dhamira ya Kweli ya kusimamia Utekelezaji wa Sera Hiyo na kuahidi kulivalia njuga Suala Hilo na kuwa (Championi) wa Utekelezaji wa Sera Hiyo.

Ameziagiza Taasisi zote za Umma na Binafsi kutekeleza kikamilifu Sera ya Biashara 2024 na tathmini ya Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara.(Zanzibar Blue Print) 2025.

Akizungumzia Uzinduzi huo wa Sera amesema itasaidia kwa kiwango kikubwa kuleta Ufanisi wa Utekelezaji wa Sekta ya Biashara na kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha Biashara.

Aidha amesema kuwa Sera Hiyo ni hatua ya Kufanikisha Ahadi ya Ilani ya CCM ya 2020-2025 ilioitaka Serikali Kuandaa Mazingira Bora ya Biashara Nchini.

Dkt, Mwinyi amewasisitiza Wadau,Sekta Binafsi na Washirika wa Maendeleo kuisoma na Kuifahamu vema na kushirikiana kufanikisha Utekelezaji wa Sera Hiyo.

Nae Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban amesema Uzinduzi wà Sera Hiyo ni safari Muhimu ya lkukuza Uchumi ,Biashara na Viwanda pàmoja na Kuimarisha Maisha ya Wananchi kwani Tayari imeonesha Udhaifu na Maeneo ya Kibiashara yanayohitaji Utatuzi wa kina.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Suleiman Said Jaffo amesema Sera Hiyo ni mwanzo Mzuri wa kulifikia Soko La Nchi za Sadic lenye Idadi ya Watu Milioni 450 na Soko la Afrika lenye Watu Bilioni 1.4 kwa ajili ya Kupata Masoko.