Jeshi la Polisi limesema kuwa linafuatilia kwa karibu tuhuma dhidi ya askari wake wawili, zinazohusishwa na kupotea kwa mwanaharakati Mdude Nyagali, kufuatia madai yaliyosambaa kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (DCP) David Misime, mwananchi mmoja ambaye bado jina lake linafuatiliwa, amewatuhumu askari hao kwamba walimfuata na kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi, wakimuahidi pia kumpatia fedha.
Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) limeunda kikosi kazi maalum ambacho tayari kimeshawasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.
Aidha, Jeshi hilo limetoa rai kwa wananchi wenye taarifa zozote zitakazosaidia katika uchunguzi huo, kushirikiana kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili kusaidia kufanikisha upatikanaji wa ukweli.
Leave a Reply