Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa onyo kali kwa mtu au kikundi chochote cha watu wenye nia ovu kutojaribu wala kuthubutu kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ikiwemo kudhuru Askari ama familia za Askari, kutokana na matamko ya baadhi ya watu na viongozi wa chama cha CHADEMA kwa kutaja baadhi ya majina ya Askari wakiwatuhumu kuhusika na tukio la kupote kwa Mdude Nyagali.
Taarifa iliyotolewa na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Benjamini Kuzaga imeeleza kwamba jeshi hilo halitasita kumchukulia hatua za kisheria na kumshughulikia mtu au kikundi chochote cha watu watakaojaribu kufanya uhalifu kutokana na matamko au kauli hizo zinazotolewa.
Itakumbukwa kwamba May 2 mwaka huu mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mpaluka Said Nyagali maarufu Mdude alivamiwa na kujeruhiwa na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake na kisha kutoweka naye kusikojulikana.
Polisi Mbeya watoa onyo kali kwa watakaojaribu kuwadhuru askari na familia zao

Leave a Reply