Aliyekuwa afisa mtendaji wa kijiji cha Kanjeme kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Julian Mkumbo (35) amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba alichokuwa akiishi mara baada ya kutoonekana kwa siku kadhaa.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP. Janeth Magomi amesema Aprili 16, 2025 marehemu alikutwa akiwa amefariki na mara baada ya uchunguzi wa awali kufanyika na madaktari walibaini kuwa sababu iliyopelekea kifo chake ni kunywa sumu ya panya.
SACP. Magomi amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo huku akitoa wito kwa wananchi na kutoa pole kwanndugu jamaa na marafiki na kuisihi jamii kumrudia MUNGU kwa imani yake na kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
Leave a Reply