Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuchunguza taarifa kuhusiana na dada yake Humphrey Polepole kuvamiwa na watu wasiojulikana na kuondoka naye.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro akizungumza kuhusu taarifa hiyo amesema kuwa siku ya jana Julai 17, 2025 Jeshi la Polisi iliziona taarifa katika mitandao ya kijamii kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni Humphrey Polepole akielezea juu ya watu kuruka ukuta maeneo ya Bahari Beach Kinondoni na kumchukua aliyefahamika baadae kwa jina la Christina Hezroni Polepole Kinyangazi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa dada huyo ambaye baadae leo Julai 18, 2025 dada huyo alifika katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa zinazohusiana na yeye kuchukuliwa na watu ambao hakuwafahamu na alidai kuwa watu hao baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyo hiyo.
Leave a Reply