Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira jijini Arusha, China Railway Construction Engineering Group Company Limited, amesheherekea kukamilika kwa hatua ya mwisho ya kumwaga zege kwenye jengo la uwanja ikiwa ni siku 360 tu tangu mkataba ulipoanza mwaka jana.
Tukio hilo limefanyika tarehe 19 julai 2025 kwenye viwanja hivyo jijini Arusha
likiambatana na kuinuliwa rasmi kwa nguzo ya paa la chuma la kwanza, ikiwa ni hatua kubwa kuelekea ukamilishaji wa mradi huo kwa hatua ya pili ya kufunika uwanja na kufanya finishing.
Kazi ya umwagaji zege imejumuisha zaidi ya mita za ujazo 50,000 za zege ambazo zimekamilika kwa ubora na vimango ndani ya miezi 8 tangu umwagaji wa zege ulipoanza rasmi. Hatua inayofuata ni uwekaji wa paa, finishing za ndani, mifumo ya teknolojia na viti.
Tukio hilo limehudhuriwa afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya mkandarasi duniani kote Bw. Wang Yefeng na viongozi wa juu wa kampuni hiyo pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Laban Kiongosi, Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma pamoja na ma DC wilaya za Arusha, wawakilishi wa wizara, wadau wa sekta ya michezo na ujenzi, ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya China na Tanzania
Ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya maandalizi ya mapema kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, ambazo Tanzania ni miongoni mwa wenyeji. Mradi huo unatarajiwa kukamilika tarehe 24 Julai 2026 hivyo kutoa muda wa kutosha wa majaribio, maandalizi na uboreshaji kabla ya mashindano ya AFCON 2027
Leave a Reply