Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited. Kikao hicho kilifanyika leo, Julai 20, 2025, huko Kizimkazi, Zanzibar.
Uongozi wa Miss World uliongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake, Bi. Julia Evelyn Morley, akiambatana na Mshindi wa Miss World 2025, Bi. Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, pamoja na Miss World Africa, Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Miongoni mwa mambo makuu yaliyojadiliwa ni pamoja na namna Tanzania inavyoweza kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Miss World mwaka 2027.

Leave a Reply