Leo Ijumaa Julai 25, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Laban Kihongosi amefanya ziara ya Kikazi Wilayani Monduli, akibainisha kuwa katika Kipindi cha Miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan jumla ya Shilingi Bilioni 46 zimetolewa kutekeleza miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo Mradi wa Maji wa Esilalei ambao umegharimu zaidi ya Bilioni 1 ukihudumia Vijiji vya Isilalei na Otukai.
Mara baada ya kukagua utekelezaji wa Mradi huo wa Maji, Mhe. Kihongosi amewaambia wananchi wa Isilalei kuwa Rais Samia anatambua Haki za Kila Mtanzania, akijua matatizo na changamoto za Watanzania, akieleza kuwa Rais Samia amemuelekeza kusimamia fedha za miradi, kuwaunganisha Wananchi wa Arusha pamoja na kuwahudumia kwa Upendo, unyenyekevu na kuwaheshimu katika kukuza ustawi wao.
Awali Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe. Fredy Lowassa kwaniaba ya wananchi wa Monduli, amemkaribisha Mhe. Kihongosi Mkoani Arusha, akimtaja kama Kiongozi mchapakazi, mwenye kutendea haki Imani ya Rais Samia ya kumteua katika nafasi mbalimbali, akitekeleza kikamilifu Ilani ya CCM na maelekezo mbalimbali ya serikali.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi wanufaika wa mradi wa Maji wa Isilalei, wamemshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka na kuwaletea mradi huo wa Maji na kubainisha kuwa awali walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma ya Maji, jambo ambalo lilikuwa likiwaweka katika hatari ya kushambuliwa na wanyamapori pamoja na mifugo yao kushambuliwa
Leave a Reply