Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufungua nanenane kanda ya Mbeya 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya wakulima (Nane Nane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yatakayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya kuanzi Agosti mosi mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa ameyasema hayo kwenye Kikao cha mwisho cha maandalizi ya maonesho ya nanenane ambapo amesema maandalizi yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 80 na kwamba maeneo yaliyobakia watakamilisha ndani ya siku chache zijazo.

Amesema maonyesho hayo kwa kanda ya nyanda za juu kusini yataanza Julai 29 lakini yatafunguliwa rasmi Agosti 1, 2025 na hivyo amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za ukanda huo pamoja na wadau kujiandaa.

Jabir Makame ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, amewataka viongozi wa halmashauri kushirikiana na wadau wengine kuwahamasisha wananchi kuhudhuria maonyesho hayo ili wakajifunze teknolojia mbalimbali za uzalishaji.

Amesema maonyesho hay oni muhimu kwa ajili ya kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi na hivyo akasisitiza kuwa ni muhimu wananchi kuhudhuria, huku afisa mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Mbeya akiwahakikishia washiriki usafiri wa uhakika.