Mgeni rasmi wa NBC Dodoma Marathon 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh milioni 100 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Tanzania Dkt. Florence Temu (wapili kushoto) iliyotolewa na Benki ya NBC .
Amref Health Africa – Tanzania imepokea msaada wa shilingi milioni 100 za Kitanzania (sawa na takribani dola 38,500 za Kimarekani) kutoka Benki ya NBC wakati wa mbio za NBC Marathon 2025 zilizofanyika Dodoma. Fedha hizo zitatumika kufadhili mafunzo kwa wauguzi 100 ili kusaidia watoto wenye changamoto ya usonji.
Mbio hizo, zilizowakutanisha mamia ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali za nchi, hazikuwa tu jukwaa la kuhamasisha afya ya mwili, bali pia fursa ya kuendeleza athari chanya za kijamii na huduma jumuishi za afya.
NBC Marathon 2025 iliyofanyika Dodoma ililenga kuimarisha mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kuboresha afya ya mama na mtoto, na kufadhili mafunzo kwa wauguzi 100 ili kusaidia watoto wenye changamoto ya usonji.
Mchango wa shilingi milioni 100 za Kitanzania (sawa na dola 38,500) utawezesha Amref Tanzania kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wa ngazi ya msingi kuhusu utambuzi, usimamizi, na utoaji wa huduma kwa watoto wenye changamoto ya usonji.
Leave a Reply