Waziri Kabudi asisitiza maadili kwa waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi mkuu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, ametaja mambo matano ya msingi ambayo sekta ya habari inapaswa kutekeleza kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, ikiwemo kuwajulisha wananchi kuhusu haki na wajibu wao, kutoa elimu juu ya sera za wagombea, kuibua na kufuatilia ukiukwaji wa sheria za uchaguzi pamoja na kuhamasisha ushiriki wa makundi maalum.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo unapaswa kuzingatia taaluma, weledi na maadili ya uandishi wa habari.