Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamsaka Moria Maarufu kwa jina la Mama Yusta , ambaye anatuhumiwa kumjeruhi Kanisia Hinju (30) mkazi wa kihulu kwa kumng’ata meno kwenye mdomo wa chini mpaka kumnyofoa kipande cha nyama kisha kukimbilia kusikojulikana baada ya kutekeleza tukio hilo.
Akitoa Taarifa hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma SACP-Marco Chilya, amesema Tukio hilo lilitokea Agosti 13, 2025 Majira ya Saa kumi za jioni katika kijiji cha kihulu, kata ya lituhi Wilaya ya nyasa, chanzo kikiwa ni ugomvi uliotokea baina ya majeruhi na mtuhumiwa huyo baada ya mtoto wa majeruhi kupigwa na mtuhumiwa kitendo kilichopelekea mama wa mtoto huyo ambaye ni kanisia Hinju kushindwa kuvumilia hali iliyopelekea ugomvi baina yao.
Halikadharika, Jeshi hilo la Polisi kupitia misako na operesheni mbalimbali limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali wakiwemo watuhumiwa saba (7) ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kipelelezi waliokamatwa wakiwa na nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo 64 ,meno ya kiboko 145,na meno ya ngiri 2 zenye thamani ya Shilingi milioni mia tatu kumi na Nne , laki sita na themanini na Mia Nne na kumi na Tisa, wakiwa wameyahifadhi kwenye mifuko ya Sandarusi kisha kuyaficha kichakani na mengine kuyafukia ndani ya shimo walilokuwa wamechimba kisha kuweka nyasi kavu kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Aidha,Jeshi hilo linamshikiria Michael Lusekero mwakifuna (50) mfanyabiashara mkazi wa Mjimwema Manispaa ya Songea kwa kosa la kukutwa na bidhaa bandia alizozitengeneza ambazo ni pombe aina ya master portable spirt chupa 9 mil 200,pombe aina ya konyagi 750ml chupa 7 ,chupa 2 za konyagi 200ml , Smat Gin 200ml chupa 3 zilizotengenezwa bila leseni pamoja na vifaa vyake alivyokiwa akitumia kutengenezea pombe hizo ambazo ni kemikali ikiwa kwenye chupa 2 ndogo zikiwa na label ya PN na Striker 6 za TRA
Leave a Reply