INEC yamtaka Mpina Kutorejesha fomu za uteuzi

Chama cha ACT Wazalendo kimepinga uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kumzuia mgombea wao wa urais, Luhaga Joelson Mpina, kurejesha fomu za uteuzi.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimepokea barua kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyoelekeza mgombea wao wa urais, Luhaga Mpina, asirudishe fomu zake, kwa kuwa Tume imepokea nakala ya barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ikitengua uteuzi wa Mpina.

ACT Wazalendo imeiomba Tume kutengua barua hiyo na kumruhusu Mpina kuwasilisha fomu zake kama ilivyopangwa awali. Taarifa ya ACT inaendelea kuisisitiza Tume kuepuka mtego wa kutekeleza majukumu yake kinyume na sheria na Katiba, na badala yake imtake Msajili wa Vyama vya Siasa awasilishe hoja zake za kupinga uteuzi wa Mpina kupitia utaratibu rasmi wa kuweka mapingamizi, hatua ambayo wanasema itatoa fursa kwa mgombea kujitetea na kulinda misingi ya haki na demokrasia.


#WasafiDigital