Mgombea wa kiti Cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kuwasafirisha watu kutoka maeneo mbalimbali ili wahudhurie mikutano ya kampeni si jambo la kushangaza wala aibu.
Akizungumza leo, Septemba 5, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Tandare, Tukuyu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Dkt. Samia alifafanua kuwa hatua hiyo inalenga kuwasaidia wananchi wanaotoka mbali kufika kwa urahisi kwenye mikutano ya chama.
“Lazima tuwasaidie usafiri wafike hapa, lakini hatutoi wilaya nyingine kwenda wilaya nyingine tunatoa ndani ya wilaya hiyo hiyo, kama wana imani ya kuja kusikiliza lazima tuwape imani ya kuwasogeza kuja kusikiliza.”
“Kwahiyo sio shida wala sio aibu kwa chama kusafirisha wanachama wake kuja kusikiliza ilani inasemaje na yale tuliyowatendea pia” – Dkt. Samia
Leave a Reply