Mgombea wa kiti Cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)na ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama wa Chama hicho kuvunja makundi ili kuelekeza nguvu kwenye hatua za Kampeni na uchaguzi mkuu 2025
Dkt. Samia ameyasema hayo Leo Sept 5,2025 katika viwanja vya Sabasaba kwenye muendelezo wa Mikutano yake ya Hadhara ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025
Dkt Samia amesema kuwa wagombea wote waliofanikiwa na hawakufanikiwa kuvunja makundi na kurudi kuwa Chama kimoja ili waingie kwenye uchaguzi wakiwa na nguvu moja
Leave a Reply