Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikili wafuasi 6 wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa kufanya mikusanyiko isiyo halali na kupanga kufanya maandamano ya kuadhimisha siku ya mashujaa wao mkoa wa Mbeya.
Taarifa ya kamanda wa Polis mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Benjamini Kuzaga imeeleza kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa September 7 huko kijiji cha Ndaga wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wakiwa njiani na kupita mmoja mmoja wakijifanya wanaelekea ibadani.
Leave a Reply