Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi zake za dhati kwa Mhe. Profesa Arthur Peter Mutharika kwa ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Malawi wa mwaka 2025.
Katika salamu zake, Rais Samia amesema anatarajia kushirikiana na Rais mteule Mutharika katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Malawi.
Aidha, Rais Samia amempongeza Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera, Chama cha Malawi Congress Party (MCP) pamoja na wananchi wa Malawi kwa kufanikisha uchaguzi wa amani na mchakato mzuri wa mpito wa madaraka.
“Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Malawi,” ameongeza Rais Samia
Prof. Peter Mutharika aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo kati ya mwaka 2014 na 2020
#WasafiDigital
Rais Samia ampongeza Mutharika kushinda Urais Malawi

Leave a Reply