SILINDE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO 2026

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David E. Silinde (Mb.), kwa Mwaliko Maalum kutoka Wizara ya Kilimo ya nchini Kenya ameambatana na Mhe.Waziri wa Kilimo wa Kenya katika ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Mombasa International Show 2026, yaliyofanyika jijini Mombasa, Jamhuri ya Kenya. Aidha,kupitia maonesho hayo Mhe.Naibu Waziri aliweza kueleza fursa mbalimbali zilizopo nchini katika Sekta Kilimo ikiwemo katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, kukuza masoko na kuimarisha fursa za biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Silinde alikutana na wafanyabiashara, wawekezaji, wasindikaji, wanunuzi, wazalishaji na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kutoka Kenya na nchi nyingine, ambapo majadiliano yalilenga namna ya kuongeza biashara na uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo.

Ushiriki wa Tanzania katika Mombasa International Show 2026 ni sehemu ya juhudi za Serikali za kutafuta na kufungua masoko ya mazao ya kilimo, kuwaunganisha wakulima na masoko, kuongeza thamani ya mazao na kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya kilimo.