Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Iringa imemhukumu Gabriel Kibasa (21) kutumikia kifungo cha Maisha jela na kulipa fidia ya shilingi Milioni Tatu kwa Mhanga baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Binti wa miaka 7 aliyekuwa akisoma darasa la pili.
Hukumu hiyo imesomwa mapema leo hii Mei 9, 2025 mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya Iringa Honorious Kando huku upande wa jamhuri ukisimamiwa na Winifrida Mpiwa pamoja na Sophia Manjoti.
Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa siku ya tukio Octoba 31, 2024 Binti huyo alikuwa ametumwa kwenda kisimani kuchota maji ndipo mshtakiwa ambaye alikuwa akichunga Ng’ombe karibu na kisima hicho akatumia mwanya huo kumvuta kichakani, kumvua nguo na kutekeleza unyama huo kisha kukimbia.
“Alichukua mdudu wake akauingiza hapa mbele kwangu alafu akasema nikimwambia mtu yeyote atanifanya kitu kibaya” Alisema mtoto huyo huku akionesha sehemu ya mbele ya mapaja yake.
Aidha ushahidi wa mtoto huyo uliungwa Mkono na Daktari aliyeithibitishia Mahakama kuwa ni kweli Binti huyo alikutwa na michubuko sehemu za siri ambazo zinaashiria aliingiliwa na kitu butu sehemu zake za siri.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa wakili upande wa jamhuri Winifrida Mpiwa aliiomba Mahakama wakati wa kutoa adhabu uzingatie kifungu cha 131 katika kutoa adhabu kwani ukatili huo umekuwa ukishamili katika Mkoa huo wa Iringa na bado umeacha kovu la kisaikolojia kwa Mhanga.
Hata hivyo mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliomba Mahakama impunguzie adhubu kwani hilo ni kosa lake la kwanza pili hana wazazi na yeye ndiye tegemeo kwa familia yake.
Baada ya Mahakama kusikilizwa pande zote mbili ikamkuta na hatia ya kosa la kubaka kinyume kifungu cha cha 130 (1) na (2) (e) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marejeo yake mwaka 2022 hivyo ikamhukumu kutumikia kifungo cha Maisha jela pamoja na kulipa fidia kwa Mhanga kiasi cha shilingi Milioni Tatu.
Ahukumiwa Jela maisha kwa Kumbaka Mwanafunzi wa darasa la pili

Leave a Reply