Watu wanne wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya Hema walilokuwa wakihamisha kugusa nyaya za umeme wa laini kubwa wakati wa shughuli ya msiba, tukio ambalo limetokea leo Disemba 24, 2024 saa 3:40 asubuhi katika Mtaa wa Ngugwini, wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi amesema waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Fredy William Mwangunda (43), Mhina Athumani Mangagwa (35), Andrew Allen Mkomwa (29), na Salehe Omary Machaky (25)
Amesema Majeruhi wa ajali hiyo ni William Gumbo (50), na Mbega Ally (49) ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya Handeni huku miili ya Marehemu ikiwa imehifadhiwa Hospitalini kwa uchunguzi zaidi.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuchukua Tahadhari za kutosha katika shughuli zinazoendana na uwepo wa nyaya za umeme ili kuepuka ajali zinazogharimu maisha na kusababisha majeraha
Leave a Reply