Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameonyesha kusikitishwa na hatua za Malawi na Afrika Kusini kuzuia mazao ya kilimo kutoka Tanzania kuingia katika nchi zao, Kupitia video aliyoipost kwenye mtandao wa Instagram leo ikionesha shehena ya ndizi za wafanyabiashara wa Tanzania zilizoharibika kutokana na zuio hilo.
Waziri Bashe amesema kuwa iwapo serikali za Malawi na Afrika Kusini hazitobadilisha maamuzi yao na kufungua masoko kwa mazao ya Tanzania ifikapo Jumatano ijayo, Tanzania nayo itachukua hatua za kusitisha usafirishaji na biashara ya bidhaa za kilimo na nchi hizo mbili.
“Hii ndio hali ambayo wafanyabiashara wetu wako nayo baada ya Serikali ya Malawi kuzuia mazao kuingia nchini kwao. Kuvumilia hili kama Serikali inayohangaika na sekta ya kilimo ni ngumu. Nafahamu kumekua na maoni mbali mbali lakini naomba niendelee kusisitiza kuwa hadi Jumatano hii inayokuja, kama Serikali za Malawi na Afrika Kusini hazitobadilisha maamuzi na kutufungulia masoko basi na sisi tutaendelea na hatua za kusitisha usafirishaji na biashara za bidhaa za kilimo na nchi hizi mbili.” – ✍️ Ameandika Waziri Bashe
Bashe: Hadi kufikia Jumatano Malawi na Afrika Kusini wasipobadili maamuzi na sisi tutasitisha

Leave a Reply