Bondia Anthony Joshua apata ajali ya Gari Nigeria

Bondia maarufu wa Uingereza na Nigeria, Anthony Joshua amepata ajali nchini Nigeria leo Jumatatu, baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori lililokuwa limesimama kando ya Barabara Kuu ya Lagos Ibadan katika Jimbo la Ogun..

Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wawili, Joshua amepata Majeraha madogo ambapo kwasasa anaendelea vizuri.

Huduma za dharura zilifika eneo la tukio kwa haraka, huku mamlaka za usalama barabarani zikianzisha uchunguzi kubaini chanzo na mazingira ya ajali hiyo.