Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitisha Mkutano Mkuu Maalum kesho Jumamosi, Julai 26, 2025. Mkutano huu, ambao utafanyika kwa njia ya mtandao, una lengo kuu la kufanya marekebisho madogo katika Katiba ya chama.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, amethibitisha taarifa hii kwa waandishi wa habari, akisisitiza kuwa maandalizi yote yamekamilika. Amesema kuwa licha ya sintofahamu iliyopo na maswali mengi kutoka kwa wananchi, anawahakikishia kuwa mkutano huo utaendelea kama ilivyopangwa.
Leave a Reply