Diamond bungeni kushuhudia uapisho wa Baba levo

Mkurugenzi wa Makampuni ya Wasafi Media, Wasafibet na WCB Wasafi, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) amehudhuria Bungeni kushuhudia uapisho wa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) Leo Nov 11,2025 Jijini Dodoma.

Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) ameshinda Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa kumshinda mpinzani wake mkubwa Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo.