Donald Trump aapishwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani

Donald Trump ameapishwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani leo, Jumatatu, Januari 20, 2025, katika sherehe iliyofanyika Washington, D.C. Hii ni mara ya pili kwa Trump kushika wadhifa huo, baada ya muhula wake wa kwanza kuanzia 2017 hadi 2021.

Katika uchaguzi wa Novemba 2024, Trump alimshinda mgombea wa chama cha Democratic, Kamala Harris, na hivyo kurejea Ikulu ya White House. Makamu wake wa rais ni JD Vance, ambaye pia ameapishwa leo.

WasafiDigital