Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu jijini Mbeya imeongezeka na kufikia wagonjwa 261 wanaopatiwa matibabu katika Kambi tatu tofauti zilizotengwa kwaajili ya kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa hao, Huku Kata ya Ilemi ikiongoza kuwa na idadi kubwa ya wagongwa.
Akitoa taarifa ya hali ya kipindupindu jijini Mbeya kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Mbeya mganga mkuu wa jiji la Mbeya Yesaya Mwasubila, amesema takwimu hizo za wagonjwa ni wale waliofika kupata huduma hadi kufikia January 6, wakati changamoto kubwa ikiwa ni jamii kuficha wagonjwa na kuchelewa kufika vituo vya kutolea huduma.
Dkt Elizabeth Nyema ni mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, anaeleza maana halisi ya ugonjwa wa kipindupindu, Huku akitoa tathmini ya ugonjwa huo kwa Mkoa wa Mbeya ambapo tayari halmashauri tatu zimeathirika na ugonjwa huo ikiwemo Mbeya jiji yenye wagonjwa wengi zaidi, halmashauri ya Chunya na halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Kwa upande wake Spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson amewaomba Wana Mbeya kujenga mazoea ya Kunawa mikono mara kwa mara na kuacha tabia ya kusalimiana kwa kushikana mikono ili kupunguza uwezekano wa kuambukizana bakteria wa ugonjwa huo.
Leave a Reply