Msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux (@juma_jux), ame-share video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiongea kwa njia ya video call na nyota wa Nigeria, Big Wiz @wizkidayo.
Katika mazungumzo yao, Jux alimuuliza Wizkid kuhusu lini atakamilisha sehemu yake ya kazi ya pamoja (collaboration), na Wizkid akajibu kwa kifupi, “Soon” yaani hivi karibuni.

Wakati huo huo, Wizkid naye alimuuliza Jux kuhusu maisha yake ya ndoa na @its.priscy 🇳🇬, jambo lililoonekana kuwavutia mashabiki zaidi.
Habari hii imepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa The African Boy (Jux), ambao sasa wanatarajia kolabo kubwa na ya kipekee kati ya Juma Jux na Wizkid, muda wowote kuanzia sasa.















Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.