Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba imethibitisha kupokea ripoti ya madaktari bingwa wa hospitali ya Sanga kuwa Padri Elipidius Rwegoshora Mshtakiwa namba moja kwenye kesi ya mauaji ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath, kuwa akili yake ni tumamu tofauti na ilivyokuwa ikielezwa.
Hayo yameelezwa na Jaji wa Mahakama hiyo Gabriel Malata kabla ya usikilizwaji wa shauri la kesi ya mauaji namba 25513 ya mwaka 2024 ya mtoto mwenye ualbino Noela Asimwe Novath inayowakabili watuhumiwa tisa,kwa hatua ya awali.
Jaji Malata amesema kuwa ombi hilo liliwasilishwa na upande wa utetezi wa mshtakiwa namba moja mnamo Oktoba 25, 2024 na Mahakama kuridhia na kutoa amri mshtakiwa huyo kupelekea Isanga kwaajili ya vipimo na kueleza kuwa baada ya kufanyika kwa vipimo, taarifa ya vipimo hivyo imesainiwa na kudhibitisha majibu hayo na daktari Enok Changalawe na tayari nakala za majibu zimekabidhiwa kwa mawakili wa mashtaka na utetezi
Jaji Malata akisoma taarifa hiyo amesema kuwa “Bwana Elpidius Rwegoshora hajaonesha dalili yoyote ya kuwa na ugonjwa au matatizo ya akili na kuwa suala la kutokuwa na akili timamu halikubainishwa kitabibu”.
Kwa upande wa Jamhuri, ukiongozwa na wakili wa serikali Ajuaye Bilishanga wameeleza kuwa kielelezo hicho cha taarifa za vipimo kitumike katika shauri hilo kwa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Washtakiwa wote tisa wamesomewa shtaka la kuuwa kwa kukusudia kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya 196 na 197 ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022, na wote kukana shtaka hilo.
Aidha katika kesi hiyo jumla ya hoja 21 za kubishaniwa na kutobishaniwa zimeibuliwa katika Mahakama hiyo na mawakili wa serikali sambamba na kueleza kuwa na jumla ya mashahidi 52, vielelezo vya maandishi 27 na vielelezo halisi 10
Baada ya usikilizwaji wa shauri hatua ya awali, Mahakama imetamka kwamba usikilizwaji umekamilika na sasa ipo tayari kusikiliza kesi ya msingi ambapo Jaji Malata ameelekeza Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kupanga tarehe na namna ya usikilizwaji wa shauri hili.
Kesi Mauaji ya Mtoto Asimwe, Padri athibitika kuwa ana akili Timamu

Leave a Reply