Baraza la madiwani la halmashauri ya jiji la Mbeya limepitisha kwa kauli moja azimio la kuligawa jimbo la Mbeya mjini ili yawe mawili wakipendekeza kuwe na jimbo la Mbeya mjini na jimbo la Uyole.
Akiwasilisha pendekezo hilo la kuligawa jimbo la Mbeya mjini kwenye kikao maalumu cha baraza la Halmashauri ya Jiji la Mbeya, afisa utumishi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Nickodemus Tindwa, amesema tayari wamependekeza majina ya majimbo hayo ambapo jimbo hilo ambapo kutakuwa na jimbo la Mbeya mjini litakua na wakazi 254,746 na jimbo la Uyole kuwa na watu 286,857.
Nje ya mkutano wa baraza hilo maalum, tumezungumza na baadhi ya madiwani ili kujua umuhimu wa kugawanywa kwa jimbo hilo ambao wamesema mgawanyo huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kusogeza mbele maendeleo kwa wananchi wa majimbo hayo.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Mbeya Mohammed Azizi Faki amewapongeza madiwani kwa kupitisha azimiohilo huku akiwashauri kujenga hoja ya kutetea wazo lao ambalo wamelipitisha na kusudio la kuligawa jimbo la Mbeya mjini.
Ikumbukwe kwamba kikao hicho maalum cha baraza la madiwani kilikuwa na lengo la kujadili barua ambayo halmashauri hiyo imepokea kutoka tume huru ya uchaguzi INEC ambayo imetoa mwanya kwa majimbo kubadili majina au kuyagawanya na kuwa na jimbo zaidi ya moja.
Leave a Reply