Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni mtia nia wa nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa ndani ya Chama hicho unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, Freeman Mbowe amesema kutwezana baina ya wanachama na viongozi wa Chama hususani katika chaguzi, hakujengi Chama Bali kufanya hivyo kunabomoa.
Mbowe amebainisha hilo Januari 13, 2025 wakati akifungua mkutano mkuu wa BAVICHA Taifa unaoendelea kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Es Salaam na kueleza kuwa kwa sasa watafanya siasa za kujenga hoja na kutetea hoja (kunyukana) lakini baada ya uchaguzi watakaa kwa ajili ya kujenga chama.
Leave a Reply