Mchakato wa Kumchagua Papa Mpya kuanza Mei 7, 2025

Baraza la Makardinali wa Kanisa Katoliki, linalojulikana kama ‘Conclave’, limetangaza kuwa mchakato wa kumchagua Papa mpya utaanza rasmi Mei 7, 2025.

Mkutano wa kumchagua Papa wa 267 utaanza baada ya kuhitimishwa kwa Misa ya Novemdiales ya kumuombea pumziko la milele Hayati Baba Mtakatifu Francisko.

Mkutano huo utafanyika katika Kanisa la Sistine la Vatikani

Jumla ya Makardinali 135 kutoka mataifa mbalimbali, wote wakiwa na umri wa chini ya miaka 80, wanastahiki kushiriki katika mchakato huo wa kumpata Papa mpya kufuatia kifo cha Papa Francis kilichotokea Aprili 21, 2025