Jeshi la polisi kwa kushirikiana na maafisa wa benki kuu Tanzania kanda ya Mbeya wanawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuendesha biashara ya upatu mtandaoni kinyume na utaratibu kupitia kampuni ya LBL.
Akitoa taarifa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa polisi ACP Wilbert Siwa, amesema jeshi hilo lilipata taarifa za uwepo wa biashara ya upatu kupitia kampuni hiyo kwa kukusanya fedha kwa wananchi kupitia mitandao kiasi cha 50,000 hadi laki tano bila kufuata utaratibu ili kuwekeza na kuwataka kuangalia video ili wapate faida kuoitia uwekezaji huo.
ACP Siwa amesema kufuatia taarifa hizo, mnamo februari 18 mwaka huu jeshi la polisi mkoa wa Mbeya walifanikiwa kufika kwenye ofisi za kampuni hiyo eneo la mwanjelwa jijini Mbeya, na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao akiwepo meneja wa LBL mkoa wa Mbeya.
Graceana Bemeye ni Kaimu Mkurugenzi BoT kanda ya Mbeya amesema shughuli zilizokua zikifanywa na kampuni ya LBL ni Kinyume na sheria namba 171 (a) ya kanuni za fedha sura namba 16 nakufanyiwa marekebisho mwaka 2022 ambayo inakataza biashara za upatu mtandaoni.
Leave a Reply