Halmashauri ya Mji Nanyamba imeupokea na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa mafanikio makubwa, ambapo jumla ya miradi 7 yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 1.7 imezinduliwa, kukaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Miradi hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya wananchi katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Nishati na Uwezeshaji wa kiuchumi.
Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa ugawaji wa viti na meza 200 kwa shule za Sekondari tano, ikiwemo Shule ya Sekondari Hinju, wenye lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Mradi wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika Shule ya Amali Chikota, unaolenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira.
Mradi wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia kwa jamii, unaolenga kupunguza uharibifu wa mazingira na athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya nishati chafu.
Mradi wa uchimbaji wa kisima cha maji chini ya ardhi katika Shule ya Amali Chikota, utakaosaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa wanafunzi na jamii jirani.
Mradi wa kikundi cha vijana cha ufyatuaji wa tofali (Manson), unaolenga kuwawezesha vijana kiuchumi na kuongeza ajira.
Mradi wa uwekaji wa umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Mtaa wa Madina, unaolenga kuongeza upatikanaji wa umeme kwa wananchi.






Leave a Reply