Kijana aliyefahamika kwa jina la Musa Solea (39) mkazi wa Kitongoji na kata ya Talaga wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ameshambuliwa kwa mshale maeneo ya ubavuni wakati akitoka shambani na mkewe huku chanzo cha tukio hilo ikidaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa hekali 100 ambazo alikabidhiwa na mahakama baada ya kushinda kesi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20.
Akizungumza akiwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akipatiwa matibabu bwana Musa amesema kuwa vitendo ambavyo amekuwa akifanyiwa na watu hao wanaohitaji eneo lake vimekuwa vikijirudia na hii ni mara ya nne amenusurika kifo tangu anunue eneo hilo.
Matinde Dotto ni Daktari kitengo cha upasuaji hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ameeleza hali ya matababu mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Kufuatia tukio hilo tumemtafuta Kamanda wa Polisi mkoani humo SACP. Janeth Magomi ambapo amethibitisha kumshikilia mmoja kati ya wanaodaiwa kufanya kitendo hicho na kutoa rai kwa wananchi kutojihusisha na vitendo hivyo kwani hakuna yeyote aliyeko juu ya sheria.
Leave a Reply