NECTA Yafuta Matokeo Ya Wanafunzi 67 Kidato Cha Nne | Watano Waandika Matusi

Baraza la Mitihani nchini (NECTA) limetangaza leo limetangaza kuyafuta matokeo yote ya watahiniwa 67 waliobainika kufanya Udanganyifu, ambapo miongoni mwao wapo Watahiniwa 5 ambao waliandika lugha ya Matusi kwenye Skripti zao kwenye mtihani huo wa Kidato cha Nne.

Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam leo Januari 23, 2025 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) Dkt Said Mohammed wakati akitoa taarifa ya Matokeo ya Kidato cha Nne Uliofanyika Novemba 2024.

” Matokeo hayo tumeyafuta kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (j) cha sheria ya Baraza la mitihani sura ya 107 ambacho husomwa na na Kifungu cha 30 (2) (b) cha Kanuni za Mtihani mwaka 2016″ amesema Dkt Said Mohammed