Nyimbo Na Mashairi Ya Tupac Kuuzwa Kwa Kiasi Cha Tsh Milioni 656.7/=.

Tovuti Ya Momenstintime.com Inauza Mashairi Na Nyimbo Za Tupac Alizorekodi Kipindi Cha Mwanzo Mwaka 1990 – 1991 Kwa Kiasi Cha Tsh Milioni 657.7/=.

Inaripotiwa Kiasi Hicho Ni Kwa Matumizi Ya Mtu Mmoja Tu Na Wakitaka ipatikane Kwa Jamii Waongeze Malipo Kwa Familia Ya Tupac Ambayo Inadhibiti Usambazaji Wa Kazi Zake Zote.

Inadaiwa 2pac Alitengeneza Album Na Kundi La “Jesse & The Kidz” Ambayo Haikutoka Kutokana Na Kifo Cha Mmoja Wa Member Wa Kundi Hilo.

Hata Hivyo Hii Sio Mara Ya Kwanza Kuuzwa Kwa Vitu Vya Tupac Kwani, Vitu Kama Pete Iliuzwa Kwa $1M (Tsh Bilioni 2.6/=), Gari Lake BMW $1.7M (Tsh Bilioni 4.4/=), Mashairi Aliyoandika Kwa Mkono Wake Ya Wimbo Wa “Tradin War Stories” Yaliwahi Kuuzwa Kwa $100K (Tsh Milioni 262.7/=).