Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza rasmi kuwa serikali yake itatambua jinsia mbili pekee: mwanamume na mwanamke. Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya kuapishwa kwa muhula wake wa pili kama Rais wa Marekani, huku likizua hisia tofauti kote nchini na kimataifa.
Katika hotuba yake, Rais Trump alisema kuwa hatua hiyo inalenga kurejesha “maadili ya asili ya kibinadamu” na kuondoa kile alichokiita “mkanganyiko wa kijinsia” katika jamii. Alisema serikali yake itasimamia sera zinazoendana na ufafanuzi wa kiasili wa jinsia, ambao unategemea viashiria vya kibaiolojia pekee.
Aidha, Rais Trump ameahidi kusaini agizo la kiutendaji litakalokataza upasuaji wa kubadili jinsia kwa watoto, kupiga marufuku watu waliobadili jinsia zao kujiunga na jeshi la Marekani, na kusitisha ushiriki wa wanaume waliobadili jinsia kushiriki katika michezo ya wanawake.
Hii ni moja ya sera za utata ambazo Rais Trump ameahidi kutekeleza katika muhula wake mpya wa uongozi, akiahidi kusimamia maadili ambayo yanaungwa mkono na wafuasi wake wengi wa kihafidhina.
Leave a Reply