Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika viwanja Bunge Jijini Dodoma tarehe 31 Mei, 2025.
Tuzo hiyo imetolewa kuenzi mchango wa Rais Mhe. Dkt. Samia katika kulitumikia Taifa na kuwaletea Wananchi Maendeleo
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Spika wa Bunge Mheshimiwa, Dkt. Tulia Ackson amesema uongozi wa Rais Samia wa miaka minne umeakisi utawala bora, weledi, uwajibikaji, uaminifu na ujumuishi.
“Umekuwa kiongozi wa mfano katika kuimarisha mifumo ya sheria, haki za binadamu, na uwazi unaozingatia usawa na maendeleo ya kila mwananchi,”alisema.
Aliongeza kuwa wanampongeza Rais Dkt. Samia kwa utumishi na uongozi wake, huku wakiamini kuwa ataendelea kuwa taa inayoangaza njia ya Taifa la Tanzania kwa miaka mingine kadhaa ijayo.
Alisema Waheshimiwa Wabunge waheshuhudia historia ya mafanikio na mabadiliko yaliyoleta tija na ustawi kwa jamii nzima.
“Leo tunapokusanyika hapa tunaadhimisha na kuutambua mchango wako kupitia Tuzo hii Maalum. Bunge la Tanzania linauenzi uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia katika kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kimaendeleo kwa ujumla wake,” alisema.
Leave a Reply