Rais wa Finland, Mhe. Alexander Stubb kufanya Ziara nchini Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Finland, Mhe. Alexander Stubb, anatarajia kufanya Ziara ya Kitaifa nchini Tanzania kuanzia tarehe 14 hadi 16 Mei, 2025 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Finland na Tanzania zina mahusiano ya miaka 60 na zimekuwa zikishirikiana katika sekta za elimu, misitu, mageuzi kwenye mifumo ya kodi, usawa wa kijinsia na maeneo mapya ya mabadiliko ya tabianchi, ulinzi, uchumi wa buluu, akili mnemba na TEHAMA.

Rais Stubb anatarajia kuwasili nchini kesho na kupokelewa rasmi na Rais Dkt.Samia Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo viongozi hao wanatarajia kufanya mazungumzo ya pamoja na kuzungumza na vyombo vya habari.

Katika Ziara hii, Rais huyo atakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo kushiriki katika Semina kuhusu Urithi wa Hayati Martti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Finland na mwanadiplomasia mbobezi aliyeshika nafasi mbalimbali ikiwemo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Namibia na Kosovo na pia aliwahi kuwa Balozi
wa Finland nchini Tanzania

Mbali na vion gozi wa kiserikali, Rais Stubb pia ameambatana na wafanyabiashara kutoka
nchini Finland ambapo atahutubia katika jukwaa la wafanyabiashara wa Tanzania na Finland linalotarajiwa kufanyika tarehe 16 Mei, 2025 ili kujadili fursa za kiuchumi na biashara baina ya nchi hizi mbili

Aidha jukwaa la wafanyabishara ltakuwa chachu ya kuchochea biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili ambapo Tanzania inategemea kunufaika na mitaji na uwekezaji kutoka Finland.

Hali kadhalika, Rais Stubb atahutubia katika semina ya vijana kuhusu masuala ya uvumbuzi itakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (NICC) iliyoandaliwa na Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Rais Stubb pia anatarajia kuzindua mradi wa Pandamiti Kibiashara (FORLAND) katika bustani ya Jiji (Botanical Gardens) pamoja na kutembelea Mradi wa Wanawake Wanaweza unaoratibiwa na UN Women uliopo Machinga Complex Ilala.

Rais Stubb atahitimisha ziara yake nchini tarehe 16 Mei, 2025 na kuagwa rasmi na Rais Dkt.Samia Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hali kadhalika, Rais Stubb atahutubia katika semina ya vijana kuhusu masuala ya
uvumbuzi itakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (NICC)
iliyoandaliwa na Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Rais Stubb pia anatarajia kuzindua mradi wa Pandamiti Kibiashara (FORLAND) katika
bustani ya Jiji (Botanical Gardens) pamoja na kutembelea Mradi wa Wanawake Wanaweza
unaoratibiwa na UN Women uliopo Machinga Complex Ilala.

Rais Stubb atahitimisha ziara yake nchini tarehe 16 Mei, 2025 na kuagwa rasmi na Rais Dkt.Samia Ikulu jijini Dar es Salaam