Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, amekamatwa leo, Januari 15, 2025, kwa tuhuma za uasi kufuatia jaribio lake la kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3, 2024 ambapo ameweka historia ya kuwa rais wa kwanza aliye madarakani nchini humo kukamatwa.
Baada ya kutangaza sheria ya kijeshi, Bunge la Korea Kusini lilimpigia kura ya kumwondoa madarakani mnamo Desemba 14, 2024. Tangu wakati huo, Yoon alikuwa amejificha katika makazi yake rasmi, akilindwa na kikosi chake cha usalama binafsi. Hata hivyo, aliamua kushirikiana na wachunguzi ili kuepusha umwagaji damu, baada ya zaidi ya maafisa wa polisi 3,000 kuzingira makazi yake.
Wachunguzi sasa wana saa 48 kumhoji Yoon kabla ya kuamua kama wataomba kibali cha kumweka kizuizini kwa hadi siku 20 au kumwachilia, Wakati huo huo, Mahakama ya Katiba inachunguza uhalali wa kumwondoa madarakani, na itaamua kama atarejeshwa madarakani au kuondolewa kabisa.
Leave a Reply