Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ikishirikiana na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), imeweka Pingamizi ili kuzuia nyumba ya Mama Mjane Bi Beatrice Tarimo isiuzwe, Baada ya Mahakama kutoa hukumu kufuatia kesi ya Fidia iliyo kuwa ikimkabili marehemu mume wake.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam Machi 13, 2025 na Mkuu wa mkoa huo Albert Chalamila, alipokuwa akielezea kuhusu hatua kadhaa zilizofikiwa na Ofisi yake katika Kumsaidia kisheria Mjane huyo ili apate haki yake.

RC Chalamila akizungumza baada ya Kuzindua Ofisi ya Machinga na Boda Boda katika eneo la Magomeni Kota, ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Twange, kuhakikisha Nyumba ya Mjane huyo haiuzwi kwa Sababu kuna Pingamizi la Kisheria Mahakamani.
“Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kwa Kushirikiana na Wanasheria wa TLS, tumeshaweka pingamizi Mahakamani ili nyumba ya Mjane huyu Isiuzwe, na nimepata Taarifa kwamba Kuna Dalali ameonekana katika nyumba hiyo leo, natoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Twange ahakikishe nyumba haiuzwi na Mjane huyu anakuwa Salama, pia mwambieni huyo Dalali aache huo mpango kwa Sababu tumeweka zuio mahakamani” amesema RC Chalamila.
Leave a Reply