Wakazi wa Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamelalamikia simu za vitisho wanazozipata kutoka kwa watu wasiofahamika, wakidai kuwa wameagizwa kwa ajili ya kuwaua huku wakiwatisha kwa kuwadai kiasi cha fedha ili kutowaua.
Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele Alhaj Majid Mwanga wakati akisikiliza changamoto za viongozi wa dini na wazee maarufu ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo husika pindi wanapopigiwa simu hizo.
Miongoni mwa kero zilizoibuliwa ni pamoja na suala la simu chonganishi, simu ambazo zimekuwa tishio kwa wananchi hao
Aidha kero nyingine iliyotajwa ni pamoja na mawakala wa kusajili line za simu kusajili simu za wengine pasipo ridhaa ya mtoa kitambulisho au namba ya NIDA.
Akijibu kero hizo Mkuu wa Wilaya ya Mlele Alhaj Majid Mwanga, amewataka wananchi hao kutoa taarifa kwenye vyombo husika pindi wanapopigiwa simu hizo.
Ametoa rai kwa viongozi wa dini kutumia fursa ya majukwaa yao kuwaelimisha wananchi pindi wanapopigiwa simu za aina hiyo kwenda kuripoti kituo cha polisi ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika.
Leave a Reply