Uamuzi kesi ya Tundu Lissu ni Mei 7, Mawakili wazidi kuvutana kisutu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Mei 6, 2025 inatarajia kutoa uamuzi wa hoja ikiwemo mapingamizi yaliyotolewa kwenye kesi ya tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya ya Kijamii ambayo inamkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu Sanjari na kupinga kesi hiyo kusikilizwa kwa njia ya mtandao.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini, baada kusikiliza hoja za pande zote kuhusiana na kuvunjwa kwa haki za gerezani za Lissu na kupinga kwa mteja wao kusomewa maelezo ya awali (PH) kwa njia ya mtandao.

Pia, upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama itoe siku 30 ili upande wa utetezi (mawakili) ukazungumze na Lissu ili akubali kuendesha kesi yake kwa njia ya Mtandao na pia umedai kwamba hakuna haki wala Katiba iliyovunjwa kwa mshtakiwa.

Ilidaiwa kuwa Aprili 3,2025 jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulaghai umma alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka “Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana , wagombea wa Chadema walienguliwa kwa melekezo ya Rais”.

Maneno mengine yalisomeka ‘ Mapolisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi, pia alichapisha maneno yaliyosomeka Majaji ni Ma-CCM hawawezi kutenda haki wanapenda wapate teuzi kuchaguliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa.

Wakati Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ikitarajia kuja na Uamuzi huo, Mei 6, 2025, pia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu inatarajia kutajwa kwa mara ya Kwanza Siku hiyo hiyo.