Tutapambana kwenye uchaguzi hatuwezi kususia – Madeleka

Mgombea Ubunge wa ACT Wazalendo, Jimbo la Kivule Peter Madeleka amesema matatizo ya barabara na maji kwa wananchi wa jimbo lake yatamalizika iwapo watamchagua yeye kuwa mwakilishi wao bungeni.

Madeleka ambaye ni Wakili kitaaluma amesema pamoja na matatizo yaliyopo katika mfumo wa uchaguzi kwa miaka mingi lakini watu makini hawawezi kususia kwasababu wananchi wakiamua kupiga kura na kulinda kura zao yeye atapata ushindi bila kikwazo.